Wimbi La Siasa

Wabunge nchini Tanzania wapitisha mageuzi ya sheria za uchaguzi

Informações:

Sinopsis

Wiki iliyopita, wabunge nchini Tanzania, walipitisha miswada mitatu ya sheria ya uchaguzi kuelekea uchaguzi mkuu mwaka ujao. Tume ya uchaguzi itabadilishwa jina na sasa itafahamika kama Tume huru ya taifa ya Uchaguzi. Mwenyekiti wa Tume na Makamu wake, watateuliwa na rais baada ya kupokea majina matatu kutoka kwenye Kamati ya usaili.Chama kikuu cha upinzani, CHADEMA kinapinga mabadiliko hayo.  Wachambuzi wetu ni Mohammed Jawadu akiwa Dar es salaam  na Hamdun Marcel akiwa Mwanza.