Afrika Ya Mashariki

Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira

Informações:

Sinopsis

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.