Afrika Ya Mashariki
- Autor: Vários
- Narrador: Vários
- Editor: Podcast
- Duración: 3:58:32
- Mas informaciones
Informações:
Sinopsis
Kwenye makala ya Afrika ya Mashariki unahabarika na kuelimika juu ya changamoto za maisha ya wananchi wa Afrika Mashariki na eneo zima la maziwa makuu. Usipitwe na Makala ya Afrika ya Mashariki kwani unapata nafasi ya kutoa mawazo yako na kusikiliza wataalamu mbalimbali watakaokuwezesha kubadili fikra na kufikia maendeleo endelevu.
Episodios
-
Tanzania:Juhudi za wabunifu katika kupunguza hewa ya ukaa kutunza mazingira
18/04/2024 Duración: 09minSerikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Masuala na Utalii, katika taarifa ya misitu na ufugaji nyuki inabainisha kuwa mkaa ni chanzo kikubwa cha nishati ya kaya katika maeneo ya mijini kwa kupikia na kupasha joto, kwa kuwa inachukuliwa kuwa ya bei nafuu na inapatikanakwaurahisi. Inakadiriwa kuwa asilimia 85 ya watu wote wa Tanzania kutegemea nishati ya majani. Nishati ya kupikia ndiyo inayoongoza kwa matumizi ya biomasi katika kaya ikilinganishwa na sekta nyingine kama vile ujenzi na kilimo sekta ya msingi.
-
Fursa za uchumi wa buluu zilizopo katika Ziwa Victoria
13/04/2024 Duración: 09minUchumi wa Buluu ni dhana pana yenye kubeba maana nzima ya kutumia kila rasilimali itokanayo na rasilimali maji kama Bahari, mito na maziwa. Dhana hii ubeba shuguli mbalimbli ikiwemo utalii, uvuvi, kilimo cha mwani, bandari pamoja na mafuta na gesi zilizomo baharini au katika maziwa.Kwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika mashariki hasa katika mikoa inayo zunguka Ziwa.Victoria kwa siku za usoni wanachangamkua fursa za uchumi wa buluu uliopo katika maeneo yao.Dhana hii inatafsiriwa kwa kasi kwa siku za usoni na imekuwa ikitajwa kama ndio mharobaini wakuwanusua wananchi walio wengi kutoa katika mnyonyoro wa umasikini uliotopea.
-
Magonjwa ya figo Afrika Mashariki
03/04/2024 Duración: 09minWagonjwa wengi barani Afrika wanahisi kuwa gharama ya matibabu ya figo ipo juu zaidi.
-
Sehemu ya pili: Mradi wa kilimo unaofadhiliwa na AFD mjini Arusha
30/03/2024 Duración: 09minMradi wa kilimo endelevu unatanua mbawa zake sio tu katika kilimo bali pia kuwajengea uwezo wakulima kufanya shuguli za ufugaji. Mradi huu unatekelezwa kwa ufadhiri wa shirika la maendeleo la Ufaransa AFD katika mkoa wa Arusha nchini Tanzania unakwenda mbali zaidi hadi kuwafikia wanamazingira.Mafuzo wanayopata wanasema yamekuwa chachu yakubadili Maisha yao kwani sasa wanamudu vyema kuwapatia Watoto wao elimu bora
-
Utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na shirika la maendeleo la Ufaransa (AFD)
20/03/2024 Duración: 09minKaribu Katika Makala ya Afrika mashariki hii leo inatuwama katika Mkoa wa Arusha palipo makao makuu ya Jumuiya ya Afrika mashariki tukiangaza juu ya miradi ya kilimo endelevu inayotekelezwa kwa ufadhili wa Shirika la maendeleo la Ufaransa AFD.
-
Changamoto zinazotokana na migumo ya wahudumu wa sekta ya usafiri Afrika
16/03/2024 Duración: 09minRaia wengi wa mataifa ya Afrika Mashariki hutegemea pakubwa sekta ya usafiri wa umma kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyengine.
-
Simulizi ya maisha ya aliyekuwa rais wa Tanzania, Hayati Hassan Mwinyi
09/03/2024 Duración: 09minHistoria ya rais mstaafu wa Tanzania, hayati Hassan Mwinyi wakati wa uhai wake.
-
Heshima aliyopewa hayati Julius Nyerere
21/02/2024 Duración: 09minMwalimu Julius Nyerere alifanya kazi kwa bidii kuona kuwa Afrika inakuwa kitu kimoja.
-
Tanzania: Simulizi ya maisha ya waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa
15/02/2024 Duración: 09minMwandishi wetu wa Mwanza Martin Nyoni anaangazia maisha ya kisiasa ya aliyekuwa waziri mkuu wa zamani nchini Tanzania Edward Lowassa.
-
Kufungwa kwa mpaka kati ya nchi za Rwanda na Burundi
09/02/2024 Duración: 09minChangamoto za kufungwa kwa mpaka kati ya Rwanda na Burundi
-
Harakati mpya za vikosi vya SADC mashariki ya DRC
31/01/2024 Duración: 09minVikosi vya SADC vinapelekwa mashariki mwa DRC kusaidia kurejesha amani. Hatua inayokuja baada ya kuondoka kwa vile vya Afrika Mashariki ambavyo vilituhumiwa na serikali ya Kinshasa kushindwa majukumu yao.
-
Muhula wa pili wa rais Felix Tshisekedi nchini DR Congo
26/01/2024 Duración: 09minMakala ya wiki hii yanaangazia ahadi za rais Felix Tshisekedi katika muhula wake wa pili kama kiongozi wa DRC.
-
Kufunguliwa kwa shule nchini Tanzania
17/01/2024 Duración: 09minWanafunzi wengi katika mataifa ya Afrika Mashariki wamerejea shuleni wiki hii.
-
Hatua Somalia kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki
01/12/2023 Duración: 09minWachambuzi wa mambo wanasema kuwa hatua ya Somalia kujiunga na EAC, itaisaidia katika vita dhidi ya makundi ya watu wenye silaha
-
Wanawake katika sanaa ya uchoraji nchini Tanzania
09/11/2023 Duración: 09minMakala ya wiki hii yanaangazia namna wanawake nchini Tanzania wamegeukia sanaa hii ya uchoraji.
-
Uelewa wa wananchi wa Mwanza kuhusu mvua za El Nino
01/11/2023 Duración: 09minBaadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki yameendelea kufanya maandalizi kuelekea mvua za El Nino.
-
Nishati inachangia asilimia kubwa kwa ukuaji wa Uchumi wa mataifa
28/10/2023 Duración: 09minSekta ya Nishati ndiyo mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa lolote lile, Mathalan takwimu zinaonesha, mahitaji ya juu ya umeme yameongezeka ambapo serikali ya Tanzania inasema kuwa muelekeo ni kuongeza katika Gridi ya Taifa MW 218.67 na kufikia MW 1,913.22 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2022/23.
-
Biashara ya samaki na dagaa jijini Mwanza nchini Tanzania.
18/10/2023 Duración: 09minMakala ya wiki yanaangazia namna wanawake waendeleza biashara ya samaki nchini Tanzania
-
Tanzania: Jamii zinavyo shiriki katika utunzaji wa hifadhi ya Ruaha
11/10/2023 Duración: 09minJamii zinavyo shiriki katika utunzaji wa hifadhi ya Ruaha
-
Juhudi za kusambaza umeme nchini Tanzania
22/09/2023 Duración: 09minZaidi ya watu milioni mia tano kusini mwa jangwa la sahara wanakabiliwa na tatizo la umeme.