Jukwaa La Michezo

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 9:44:13
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali. 

Episodios

  • Namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa kutoka Olimpiki ya Paris

    17/08/2024 Duración: 24min

    Jumamosi hii tumezungumzia namna wanariadha wa Afrika walivyopokelewa na mataifa yao kutoka Olimpiki ya Paris, michuano ya klabu bingwa Afrika imeanza kusaka tiketi ya hatua ya makundi, uhamisho tata wa wachezaji wa soka nchini Kenya huku ligi za Afrika Mashariki na Ulaya zikianza kurejea, Mbappe ashinda taji la kwanza Real Madrid, Pochettino kuwa kocha wa Marekani

  • Paris Olimpiki: Tamirat Tola kutoka Ethiopia ndiye mshindi wa mbio za marathon

    10/08/2024 Duración: 19min

    Tuliyokuandalia Jumamosi hii kutoka taasisi ya Alliance Francaise, ni pamoja na uchambuzi wa matokeo ya marathon, riadha na mashindano mengine ya Olimpiki ya Paris yaliyotukia wiki hii. Pia tunaangazia fainali kubwa zinazosubiriwa jioni ya leo na kesho asubuhi kwenye marathon ya kina dada lakini pia kifo cha aliyekuwa rais wa tano wa shirikisho la soka Afrika CAF, Issa Hayattou.

  • Jukwaa La Michezo: Fainali ya mita 100 kwa wanaume yasubiriwa, Olimpiki Paris

    04/08/2024 Duración: 23min

    Tuliyokuandalia ni pamoja na matokeo ya Olimpiki hapo jana raia wa St Lucia Julien Alfred akishindia taifa lake medali ya kwanza ya Olimpiki, Sudan Kusini yaaga mashindano ya basketboli kibingwa, uchambuzi wa wanariadha wa Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki nusu fainali na fainali kadhaa leo usiku na kesho, uchambuzi wa mechi za nusu fainali ya soka lakini pia kwenye mjadala tunazungumzia kashfa ya jinsia ya mabondia Angela Carini na Imane Khelif

  • Jukwaa La Michezo: Cheptegei aishindia Uganda medali ya kwanza Olimpiki ya Paris

    03/08/2024 Duración: 23min

    Joshua Cheptegei ashinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 10,000 huku Malkia Strikers ikibanduliwa mashindanoni. Morocco na Misri zafuzu nusu fainali huku waafrika kwenye uogeleaji wakifanya vibaya. Pia tutakufahamisha matokeo ya judo, basketboli, kuendesha basikeli na jedwali la medali ambapo Uchina inazidi kuongoza jedwali hilo

página 2 de 2