Changu Chako, Chako Changu

Informações:

Sinopsis

Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.

Episodios

  • Historia ya kabila la Wadigo wa Kenya na Tanzania katika Makala Changu Chako na Florence Kiwuwa

    28/11/2023 Duración: 20min

    Katika Makala haya,Florence Kiwuwa mtangazaji wa maswala ya Historia na utamaduni kutoka RFI Kiswahili anakuletea historia ya wadigo wa Kenya na Tanzania  na kwenye le Parler francophone tutaangazia kuhusu maonyesho yake Dj Click katika ukumbi wa  Alliance Francaise ya Arusha nchini Tanzania. Na kwenye Muziki tutamuangazia mwanamuziki Koffi Olomide kutokea DRC.

  • Tamaduni za watu wa Katanga katika uchimbaji wa madini na msanii Masauti kutoka nchini Kenya

    19/11/2023 Duración: 19min

    Ni furaha kubwa kukutana nawe kwa mara nyingine tena katika Makala haya Changu Chako Chako Changu ambapo leo nitaungana na mwenzangu DENISE MAYO kukujuza kuhusu tamaduni za watu wa huko Katanga katika uchimbaji wa madini, kwenye le parler francophone nitakujuza ratiba wa Alliance francaise za Ukanda na Institut Français ya Lubumbashi, kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Kutoka nchini Kenya Mohammed Ali Said, anaefahamika sana kama Masauti. Mimi ni Ali Bilali

  • Utamaduni wa kabila la Wataita na mwanamuziki Hiro le Coq katika Makala haya ya leo.

    13/11/2023 Duración: 19min

    Karibu mpenzi msikilizaji katika Makala ya leo Changu Chako Chako Changu, ambapo nakukumbusha historia na tamaduni ya watu wa kabila la wataita, na kwenye le parler francophone tutaangazia ratiba ya shughuli za kitamaduni Alliance France Francaise ya Nairobi, Dar es salaam, Arusha, na Institut francais ya Lubumbashi. Na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Hiro Le Coq rapa wa Ufaransa mwenye asili ya DRC. Mimi naitwa Ali Bilali bienvenue.

  • Mwanahabari kutoka DRC ashinda Toleo ka kumi la tuzo Ghislaine Dupont na Claude Verlon

    09/11/2023 Duración: 19min

    Makala haya yanazungumzia kuhusu tolea la 10 la tuzo ya Ghislaine Dupont na Claude Verlon ambalo hutolewa kila Novemba 02 ya kila mwaka na RFI ili kuwaenzi waandishi wa habari hao wawili waliofariki miaka 10 iliopita huko Kidal kaskazini mwa Mali baada ya kutekwa na wanajihadi, ambapo Joseph Kahongo wa (RDC) na Ange J. Agbla (Bénin) ndie washindi wa toleo hili la kumi. ambatana naye Ali Bilali kudahamu mengi zaidi.

página 2 de 2