Sinopsis
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
Episodios
-
Uzazi wa Mpango:Wanaume wajitolea kufanya upasuaji wa mirija -Vasektomia
31/12/2024 Duración: 09minVasectomy ni njia ya kupanga uzazi ambayo inahusisha upasuaji wa mshipa unaopitisha mbegu za kiume, ili mme asiweze kumpachika mke mimba. Ni njia ya upangaji uzazi ya milele.Na pengine unajiuliza hili linafanyiikaje na ina athari gani kwenyen afya ya mwanaume ?Sikiliza makala haya
-
Kupanga uzazi kwa kutumia njia za homoni na ile ya Kitanzi -Matatizo ya Afya kwa Wanawake
24/12/2024 Duración: 10minKwenye awamu yetu ya Kwanza tuliangazia njia za asilia walizokuwa wanatumia nyanya zetu kabla ya sayansi kuingia.Tukataja njia ya Kalenda,mipira ya kondomu na kumwaga mbegu za kiume nje ya njia ya uzazi almaarufu Withdrawal.Hivyo basi kwenye sehemu hii ya pili tutaangazia njia za homoni na zisizo za homoni na ambazo asilimia kubwa ya wanawake wanatumia.Kama vile vidonge, vipandikizi ,sindano, na IUD.
-
Uzazi wa mpango kwa njia asilia
17/12/2024 Duración: 09minMakala haya yanaangazia upangaji kupanga uzazi, na jinsi linavyohusiana na afya ya mwanamke. Kupanga uzazi ni sehemu muhimu ya afya, kwani husaidia wanawake kudhibiti idadi ya watoto wanapokuwa nayo, na pia ina athari kubwa katika afya yao ya kimwili na kihisia.
-
Juhudi za kupunguza matumizi ya dawa za kulevya eneo la Pwani ya Kenya
13/12/2024 Duración: 10minIdadi ya vijana wanaotumia dawa za kulevya katika umri mdogo imeongezeka
-
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani
09/12/2024 Duración: 09minKatika makala haya, tutazungumza na watu muhimu kama vile mgonjwa wa UKIMWI, daktari, na mkunga anayeelimisha kuhusu jinsi ya kuzuia watoto kuambukizwa virusi vya UKIMWI wakati wanapozaliwa. Pamoja, tutafahamu changamoto, mafanikio na hatua zinazochukuliwa katika vita hivi.
-
Dunia: Wahudumu wa afya waendelea kuuawa katika maeneo ya mizozo
07/12/2024 Duración: 10minUmoja wa mataifa umeorodhesha mwaka 2024 kama mwaka hatari zaidi kwa wafanyikazi wa mashirika ya kimsaada Katika takwimu za UN ,wafanyakazi zaidi ya 200 wamewauwa katika mzoz wa Gaza na wengine zaidi ya 20 katika mzozo wa Sudan
-
Afya ya kujifungua na uzazi: Changamoto zinazotokea wakati wa kujifungua mtoto
12/11/2024 Duración: 10minIdadi kubwa ya kina dada wameamua kuchagua upasuaji kama njia rahisi ya kujifungua kwa sababu tofauti tofauti.Sehemu ya pili ya makala haya inaangazia ni kwa nini idadi hio inaongezeka kisha hali inakuaje pale kwenye chumba cha kujifungulia.Dakatari Lilian Nkirote kutokea hospitali ya Jacaranda jiji Nairobi anaelezea kwa kina.
-
Afya ya uzazi na kujifungua
08/11/2024 Duración: 10minMakala ya siha njema wiki hii tunaangazia Afya ya uzazi na kujifungua na sio safari nyepesi.Ni safari yenye changamoto haba na furaha kwa wanawake na familia zao. Ni muhimu kwa kila mama mjamzito kufahamu hatua muhimu za kuhakikisha ustawi wa afya yake na ya mtoto anayemtarajia. Kupitia huduma bora za kiafya na ushauri wa wataalamu, wanawake wanaweza kufurahia safari ya uzazi kwa usalama na utulivu.
-
Juhudi za kikanda kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka
29/10/2024 Duración: 08minKumekuwa na mikakati maksudi katika nchi za Afrika kuwekeza katika utafiti kuhusu nyoka na matibabu ya simu yake Baadhi ya mikakati hiyo ni utafiti wa kuwa na aina moja ya dawa ambayo inaweza kutumika katika nchi za Afrika Mashariki vile vile kuelimisha jamii kuhusu huduma za kwanza sahihi kuwasaidia wagonjwa na namna ya kuzuia madhara zaidi kutokana na sumu ya nyoka.
-
Kukabiliana na tatizo la kiafya la kungatwa na nyoka katika ukanda wa Afrika
22/10/2024 Duración: 10minKungatwa na nyoka imeorodheshwa miongoni mwa matatizo ya kiafya yaliyotengwa Takwimu za shirika la afya duniani ,WHO zinasema kila dakika nne ,watu nne duniani, hupoteza maisha kutokana na sumu ya nyoka.Hii ni kutokana na gharama ya juu ya matibabu ,ugumu wa kupatikana na matibabu haya na raia kutofahamu hatua sahihi ya kufuata ukiumwa au kutemewa sumu na nyoka.Nchini Sudan Kusini ,visa vya wagonjwa wanaongatwa imeongezeka maradufu kutokana na mafuriko ya miezi kadhaa kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka,MSFMSF hata hivyo kudhibiti hali ,inatumia mfumo wa akili mnemba au AI kurahisisha ubainishaji wa ainya ya nyoka na sumu yake vile vile matibabu yake,mradi unaoendeshwa na MSF katika baadhi ya vituo vyake jimbo la Warrap na Abyei.
-
ICRC yapambana kutoa huduma za afya za dharura ndani ya saa 96
08/10/2024 Duración: 10minKamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu,ICRC mara nyingi hubidi kuhudumu katika maeneo yenye mizozo kutoa huduma za dharura ,msaada wa kibinadaam ikiwemo afya Ili kukabiliana na changamoto za kuafikia malengo yake ya kutoa huduma za afya za dharura katika uwanja wa vita ,maeneo yenye majanga ,imebidi kufumbua mbinu ya kuwa na hospitali za muda ambazo zinajengwa kutumia hema na zinaweza kufanya kazi ndani ya saa 96ICRC inaendelea na mafunzo ya kuwaandaa wahudumu wa afya wanaohudumu katika mazingira hatarishi ,ili wapate kuhudumu ipasavyoMafunzo hayo yanatolewa kwenye hospitali halisi ambazo hutumika katika maeneo ya mizozo ,ambapo wahudumu hao hutakiwa kushughulikia mazingira tofauti ya dharuraMafunzo hayo yamefanyika nchini Kenya mara mbili ambapo wahudumu hao kutoka maeneo tofauti wanawekwa kwenye makundi na kutakiwa kutangamana na kushughulikia dharura tofauti kabla kuanza kutumwa kwenye maeneo ya mizozo
-
-
Ubunifu kutatua changamoto za miundombinu kwenye usafi na maji taka
24/09/2024 Duración: 10minMashirika ya nchini Kenya kwa ushirikiano na serikali za kaunti ,yamezindua mfumo mpya na wa kisasa wa vyoo bunifu visivyotumia maji wala kuunganishwa na mabomba ya maji taka Hatua Ambayo imeonekana kupunguza msambao wa magonjwa kama vile kipindupindu.
-
Ukosefu wa Ufahamu wa haki za afya ya uzazi ni kikwazo kikubwa ukanda wa Afrika
17/09/2024 Duración: 10minRaia wengi bado hawawezi kufurahia haki zao za afya ya uzazi kutokana na ukosefu wa ufahamu Haki hizo ni pamoja na haki ya kuwa mzazi au la,kupata habari kuhusu afya ya uzazi ,kupata huduma bora za uzazi ,kushiriki mapenzi kwa njia stahiki na kuhudumiwa katika vituo vya afya kwa heshima
-
Matatizo ya kupata uja uzito miongoni mwa wanafamilia yanazidi kuongezeka
03/09/2024 Duración: 10minRipoti nyingi zinaonesha wanawake pamoja na wanaume wanakabiliwa na changamoto za uzazi Wanandoa nyingi wanalazimika kukaa miaka mingi kabla kupata watoto ,kitu ambacho bado kinazingatiwa na jamii za Afrika kuwa ukamilifu katika kila ndoa au familia.Daktari bingwa wa uzazi dkt Dennis Miskella anaeleza juhudi za kutafuta mtoto zinastahili kuwa ushirikiano kati ya mke na mumeweBaadhi ya sababu zinazohusishwa na hali hii ni kushiriki tendo la ndoa visivyo ,athari za baadhi ya mbinu za kupanga uzazi ,uvutaji sigara na pia unene wa kupitiliza
-
Wanawake wawafuga samaki kukwepa msambao hatari wa Ukimwi ziwa Victoria
28/08/2024 Duración: 09minMashirika ya kiraia yanayofanya kazi maeneo ya Kisumu nchini Kenya wanawasaidia wanawake kuachana na mpango wa kuuza miili yao ili kupata samaki Tabia hiyo inayofahamika kama ngono samaki kwa wakazi imekuwa ikichangia msambao wa virusi vya HIV
-
WHO imetoa mwongozo wa kupambana na MPOX katika mataifa ya Afrika
20/08/2024 Duración: 10minMikakati ambayo WHO inahimiza nchi za Afrika kukumbatia ni ubadilishanaji wa taarifa kuhusu ugonjwa wa Mpox ,ubainishaji sahihi na kampeni za chanjo Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ,kuna hofu ya msambao hatari wa MPox unaohuishwa na vitendo vya ngonoWatalaam wa afya nchini DRC pia wanahimiza uhamasisho zaidi kuhusu ugonjwa huo ambao umesababisha vifo zaidi ya 500
-
MPOX yatangazwa janga la dharura la kiafya baada ya kasi ya maambukizi kuzidi
20/08/2024 Duración: 09minShirika la afya duniani ,WHO na taasisi ya kudhibiti magonjwa ya umoja wa Afrika ,CDC zililazimika kuchukua uamuzi mzito wa kutangangaza MPOX dharura ya kiafya Mataifa 16 ya Afrika kati ya 55 yameripoti visa vya MPOX mwaka huu ,CDC ikisema maambukizo yamepanda hadi asilimia 160 mwaka huu ukilinganishwa na mwaka 2023Virusi vya MPOX vimeripotiwa kujibadilisha na kwa sasa msambao hatari wa virusi sugu zaidi unahusishwa na ngono
-
Bidhaa mpya za tumbaku zinauzwa kwa mwoneko bora, ladha ya kuvutia kuficha madhara yake
06/08/2024 Duración: 09minKuuza bidhaa za tumbaku za kisasa ,kama bidhaa zisizo na madhara ,kutumia ladhaa tamu na kutumia mitandao ya kijamii kuuza bidhaa hizi ni mbinu ambao kampuni za kutengeneza tumbaku zinatumia kuwavutia vijana na kuwa wateja wao wa kudumu. Kampuni hizi zinafadhili pia utafiti ambao unakinzani na utafiti wa taasisi za afya kuhusu madhara ya Tumbaku.Isitoshe kampuni hizi zinazalisha bidhaa ambazo mtumiaji anaweza kutumia zaidi ya moja .
-
Mbinu fiche zinazotumia sekta ya kuzalisha tumbaku kuendelea kudumu soko
01/08/2024 Duración: 10minKumeshuhudia juhudi makhsusi kutoka sekta ya Tumbaku zinazopinga sheria zinazodhibiti Tumbuka kama vile kupitia ushuri au sheria zenye adhabu kali Sekta hii pia imeonekana kurubuni serikali tofauti kwa kutoa msaada bila wao kufahamu lengo la sekta hiyo. Aidha kuna tafiti za kisayansi zinazofadhiliwa na sekta hii kukabili sayansi zinazorodhesha tumbaku na bidhaa za sigara kuwa zenye madhara makubwa ya kiafya