Gurudumu La Uchumi

Informações:

Sinopsis

Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .

Episodios

  • Wataalamu: Uchumi Samawati utumiwe vizuri kwa maendeleo endelevu

    11/04/2024 Duración: 10min

    Kulingana na Benki ya Maendeleo ya Afrika, uchumi wa bluu barani Afrika una uwezo wa kuchangia pakubwa katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya bara hilo.Uchumi wa bluu unatajwa kuchangia dola za Marekani trilioni 1 kila mwaka, Sekta ya uvuvi ikiwa kitovu kikuu na kuajiri zaidi ya watu milioni 12.Profesa Omary Mbura, mtaalamu na mhadhiri wa masuala ya uchumi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, anaangazia sekta hii. 

  • Umuhimu wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na uma

    04/03/2024 Duración: 10min

    Shughuli za sekta binafsi na uwekezaji ni vyanzo vikuu ya ukuaji wa uchumi, uzalishaji wa ajira na maendeleo endelevu.Kwa wastani, sekta binafsi inachangia zaidi ya Asilimia 80 ya mapato ya serikali kwa watu wa kipato cha chini na cha kati, kupitia kodi ya kampuni, kodi ya rasilimali na mapato ya kodi kwa wafanyakazi.Sekta hii inazalisha zaidi ya asilimia 90 ya ajira katika nchi zinazoendelea kiuchumi.

  • Ukulima wa matunda Kenya na changamoto zake

    04/03/2024 Duración: 10min

    Makala ya Gurudumu la Uchumi, juma hili inaangazia kilimo cha matunda nchini Kenya, na namna wakulima wa nchi hiyo, wameendelea kukumbatia mbinu mpya za kilimo, uvunaji na usindikaji.

  • Changamoto za uhamiaji na fursa zake kwa uchumi

    04/03/2024 Duración: 10min

    Uhamiaji unaweza kuwa nguzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Afrika ikiwa mtu anaweza kutoa mwelekeo bora wa fedha zinazotumwa na wageni kuelekea uwekezaji na ufadhili wa maendeleo katika nchi za Afrika.Diasporas wanachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi zetu ambazo kimsingi ni nchi za asili lakini pia nchi mwenyeji. Wanafanya hivyo kwa kuhamisha pesa, ujuzi, teknolojia, mifano ya utawala, maadili, na mawazo. Serikali ya Senegal inafahamu mabadiliko yanayohitajika tunapojitahidi kutekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na Mkataba wa Kimataifa wa Uhamiaji Salama, Ulio na Utaratibu na wa Kawaida nchini Senegali.

  • Kuberoshwa kwa huduma ya intaneti Kenya na ilivyochochea ubunifu

    04/03/2024 Duración: 10min

    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, tunaangazia namna maboreshi ya huduma ya Inteneti nchini Kenya imechochea maendeleo, biashara na ustawi wa watu. 

  • Mzozo kati ya Kenya na Tanzania kuhusu mashirika yake ya ndege

    04/03/2024 Duración: 09min

    Msikilizaji, hatimaye nchi ya Tanzania imeondoa zuio ililoweka juma hili kwa ndege za shirika la Kenya KQ, uamuzi iliyokuwa imeuchukua baada ya Nairobi kukataa kutoa kibali kwa ndege za mizigo za shirika la Tanzania kushusha na kupakia kutokea Kenya.Uamuzi huo msikilizaji ulisababisha mawaziri wa pande zote kukutana na Jumanne ya wiki hii wakakubaliana kumaliza tofauti zilizojitokeza na sasa safarai za ndege za Kenya na zile za Tanzania zitaruhusiwa. 

  • Mustakabali wa Jumuiya mwaka 2024

    04/03/2024 Duración: 09min

    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.

  • Matarajio ya Wafanyabiashara kwa mwaka 2024

    04/03/2024 Duración: 09min

    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, inaangazia namna wafanyabiashara wamejipanga katika mwaka 2024, kuhakikisha biashara zao zinashamiri licha ya changamoto za kiuchumi zinazoikabili dunia kwa sasa. Mwandishi wetuj Victor Moturi, kwa niaba ya mtayarishaji wa makala haya, Emmanuel Makundi, amezungumza na wafanyabiashara nchini Kenya, ambao mwaka uliopita, walilalama kupata changamoto za kifedha na hata upandaji wa bidhaa na kukosekana kwa dola.

  • Matarajio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2024

    11/01/2024 Duración: 09min

    Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia mustakabali wa jumuiya ya Afrika Mashariki kiuchumi kwa mwaka 2024, hasa baada ya athari za uviko 19 za tangu mwaka 2020 na sasa mdororo wa uchumi wa dunia, ambao umesababisha mataifa masikini, ikiwemo ya ukanda kushuhudia kupanda kwa gharama ya maisha.Nimezungumza na Johnson Denge, mchambuzi wa masuala ya uchumi akiwa nchini Kenya.

  • Mkutano wa China na Afrika pamoja na ziara za viongozi nchi za Magharibi barani Afrika

    02/11/2023 Duración: 09min

    Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili inaangazia mkutano wa nchi ya Uchina na viongozi wa Afrika uliofanyika wiki kadhaa zilizopita, pamoja na ziara za viongozi wa nchi za Marekani, Uingereza na Ujermani kwenye nchi za Afrika Mashariki na Magharibi.Ziara zao zinaashiria nini katika muktadha wa kiuchumi? Emmanuel Makundi amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, kuangazia haya kwa kina.

  • Kwanini Bostwana imefanikiwa kwenye sekta ya madini ?

    25/10/2023 Duración: 08min

    Kwenye sehemu yetu ya pili na ya mwisho kuhusu namna nchi ya Bostwana ilivyopiga hatua kwenye sekta ya madini na uchumi wake kwa kutegemea Almasi, tutasikia kutoka kwa wadau mbalimbali akiwemo mwekezaji  binafsi Siddarth Gothi , Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo KGK Bostwana, na mchambuzi binafsi wa siasa, Marisa Lourenco, kutoka Afrika Kusini   kuhusu mafanikio hayo lakini pia changamoto katika sekta hiyo.

  • Fursa za uwekezaji nchini Bostwana kwa nchi za Afrika Mashariki

    20/10/2023 Duración: 09min

    Kati ya Oktoba 11 hadi 14 mwezi Oktoba, Bostwana iliandaa maonesho ya Kimataifa ya kibiashara jijini Gaborone, yaliyofanyika pembezoni mwa Jukwaa la kwanza wa kibiashara kati ya nchi hiyo na Umoja wa Ulaya. Bostwana ambayo uchumi wake mkubwa unategemea sekta ya madini, hasa Almasi ikiwa ya pili duniani kwa bidhaa hiyo baada ya Urusi, ilitumia fursa hiyo kujitangaza na kuvutia wawekezaji zaidi.Nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha juu kufikia 2036 kwa kupanua uchumi wake kwenye sekta nyingine kama kilimo na utalii, ni miongoni mwa mataifa duniani, ambayo taasisi za Kimataifa kama IMF na Benki ya dunia, zinasema uchumi wake unakuwa kwa kasi.Je, Bostwana ina fursa zipi za uwekezaji hasa kwa mataifa ya Afrika Mashariki ? Wakati wa maonesho hayo, nilitembelea banda la Kenya, na leo kwenye Makala yetu ya Gurudumu la Uchumi, utamsikia Balozi wa Kenya nchini Bostwana.

  • IMF, benki ya dunia zaonya kuhusu kudorora kwa uchumi wa mataifa ya Afrika

    11/10/2023 Duración: 09min

    Ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara, unatarajiwa kupungua kasi mwaka huu, kutokana na kudorora kwa uchumi wa mataifa ya Afrika Kusini, Nigeria na Angola, hii ni kwa mujibu wa ripoti ya Benki ya Dunia.Ukuaji wa kikanda utapungua hadi 2.5% mwaka 2023 kutoka 3.6% mwaka jana, imesema ripoti hiyo.Mtayarishaji amezungumza na Johnson Denge, mtaalamu na mchambuzi wa masuala ya uchumi, kuangazia ripoti hizi kwa kina. Aidha kwa mujibu wa IMF Uchumi wa dunia unakua lakini sio kwa kasi, ambapo inakadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa dunia utapungua kutoka asilimia 3.5 mwaka 2022 hadi asilimia 3 mwaka huu na asilimia 2.9 mwaka ujao. IMF inasema Mfumuko wa bei ambao haujumuishi bei ya chakula na nishati pia unatarajiwa kupungua, ingawa polepole zaidi. Nchi nyingi zikitajwa kutokuwa na uwezekano wa kurudisha mfumuko wa bei hadi 2025.

  • Viongozi wa dunia wajadili malengo endelevu ya umoja wa Mataifa

    05/10/2023 Duración: 09min

    Mwezi uliopita, viongozi wa dunia walikutana jijini New York, Marekani katika mkutano wa 78 wa baraza la umoja wa Mataifa, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ikiwemo usalama wa dunia na ukuaji wa uchumi pamoja na mikakati ya kufikia ajenda ya mwaka 2030 na haja ya kuongeza kasi kutekeleza malengo 17 endelevu. Kuzungumzia yaliyojiri, mtayarishaji wa makala haya alimualika Ebenezer Suleiman Mathew Ikomba, balozi wa vijana wa Tanzania kwenye umoja wa Mataifa. Katika mijadala mingi, vijana walitajwa kuwa sehemu kubwa ya nguvu kazi ya dunia na kwamba kupitia ubunifu, uwajibikaji na harakati za kuhamasisha nchi kufikia malengo endelevu, basi dunia itakuwa sehemu salama. Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia yaliyotokana kwenye mkutano huo na namna gani vijana wanaweza kushiriki katika ujenzi wa dunia salama na yenye amani ambayo itachochea maendeleo na ukuaji wa uchumi. 

  • Tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki

    22/09/2023 Duración: 09min

    Katika Makala ya Gurudumu la Uchumi juma hili, mtayarishaji wa makala haya amezungumza na Profesa Wetengere Kitojo, mtaalamu wa masuala ya uchumi akiwa Tanzania, ambapo wanaangazia kuhusu tatizo la uhaba wa dola ya Marekani kwenye nchi za Afrika Mashariki. 

  • Biashara ya madini yaimarika nchini DRC

    07/09/2023 Duración: 09min

    Wiki hii tunaangazia huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako kunaripotiwa ongezeko kubwa la uzalishaji wa madini ya shaba na kobalt katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Takwimu kutoka sekta ya madini, zinaonesha kuwa uzalishaji wa kobalt imeongezeka na kufikia zaidi ya Tani Laki moja, baada ya serikali kuwekeza asilimia 43 ya bajeti yake ya taifa kwenye sekta hiyo. Kwenye Makala haya, mwandishi wetu wa Lubumbashi Denise Maheho, amezungumza na watafiti wa madini na mashirika ya kiraia, katika eneo la Katanga.

  • Nguo za mitumba zapigwa marufuku nchini Uganda

    01/09/2023 Duración: 09min

    Serikali ya Uganda imepiga marufuku uingizwaji na uuzwaji wa nguo kukuu maarufu kama mitumba nchini humo. Rais Yoweri Museveni anasema, hatua hiyo itasaidia kukusa viwanda vya ndani vya nguo na kuunda ajira hasa kwa vijana. Mwandishi wetu wa Kampala Kenneth Lukwago anatueleza zaidi.

  • MABADILIKO YA TABIA NCHI KWA UCHUMI

    10/08/2023 Duración: 10min

    Athari za mabadiliko ya tabia nchi kuanzia mafuriko na ukame zimesababisha mamilioni ya raia kupoteza makazi yao, wengi wakitumbukia katika hali ya umasikini na hata kufa njaa, baadhi wakikosa huduma muhimlu ya afya, elimu huku tofauti kati ya walionacho na wasionacho ikiendelea kuongezeka, uchumi wa mataifa ukidorora. Kwa mujibu wau moja wa Mataifa mpaka kufikia mwaka 2030 watu wanaokadiriwa kufikia milioni 700 huenda wakawa wakuhamahama kutokana na ukame peke yake.Kuchukua hatua stahiki kukabili mabadiliko ya tabia nchi na athari zake ni jambo lisilohitaji mjadala wa muda mrefu ili kunusuru maisha ya raia pamoja na kufikia malengo endelevu ya umoja wa Mataifa.Haya yanajiri wakati huu joto likiendelea kuongezeka, nchi zikitumia fedha nyingi kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi badala ya kuwa zingeelekezwa katika kutatua changamoto za maendeleo na kiuchumi hasa kwenye nchi masikini.Makala ya Gurudumu la uchumi juma hili, inaangazia ni namna gani nchi zinazoendelea zinaweza kukabiliana na athari z

  • Je Afrika inawezaje kutumia raslimali watu kwa maendeleo ya uchumi?

    02/08/2023 Duración: 10min

    Takwimu zinaonyesha kuwa rasilimali watu katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara, ilikuwa ndogo mno ikilinganishwa na mataifa mengine ya dunia, ambapo Uviko 19 na vita vya Urusi nchini Ukraine vilichangia.  Wiki hii Emmanuel Makundi anaangazia wito wa wakuu wa nchi za ukanda ili kuangalia namna bora zaidi ya kutumia nguvu kazi iliyoko barani Afrika kwa maendeleo.

  • DRC: Kushuka kwa thamani ya fedha na changamoto la wakimbizi wa ndani

    26/07/2023 Duración: 09min

    Wimbi la wakimbizi wa ndani pamoja nakushuka kwa thamani ya pesa za kongo dhidi ya dola za Marekani  kumesababisha kupanda kwa gharama za maisha katika miji kadhaa nchini jamuhuri yakidemokrasia ya Kongo. Makal aya Gurudumu la uchumi juma hili inaangazia kwa kina hali hii na mtayarishaji Emmanuel Makundi, ameshirikiana na mwandishi wa Goma Benjamini Kasembe pamoja na kuzungumza na mtaalamu wa uchumi kutoka Bukavu Bengeya Machozi.

página 1 de 2