Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 134:18:54
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodios

  • Taarifa ya habari:Tume ya kifalme yazinduliwa kuchunguza chuki dhidi ya wayahudi

    09/01/2026 Duración: 09min

    **WAZIRI MKUU ANTONY ALBANESE AZINDUA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA TUME YA KIFALME YA KUCHUNGUZA KESI ZA CHUKI DHIDI YA WAYAHUDI AUSTRALIA. **MAWIO YA MOTO YAWEKWA SEHEMU MBALIMBALI AUSTRALIA HUKU JOTO IKIZIDI KUONGEZEKA ** KIFO CHA MWANAMKE MAREKANI YAZUA UTATA.

  • Yaliyojiri Afrika:kapteni Ibrahim Traore anusurika jaribio jingine la mapinduzi

    08/01/2026 Duración: 09min

    Kwa habari au maelezo zaidi tembelea sbs.com.au/swahili.

  • Afya:wataalamu waonya dhidi ya madhara ya kuchanganya mipango mbalimbali ya lishe

    08/01/2026 Duración: 09min

    Mipango ya lishe kama vile Foodmap, yenye protini nyingi, isiyo na gluten, yenye mafuta kidogo, na kula chakula safi - kuna mipango mingi sana ya lishe, na ushauri unaokinzana. Wataalamu wa Australia wanaonya kwamba kufuata mipango mbalimbali ya lishe kwa wakati mmoja kunaweza kuwa na matokeo yasiyotarajiwa.

  • Makala leo:wazazi wapata afueni baada ya serikali kupunguza gharama za vituo vya malezi ya watoto

    08/01/2026 Duración: 05min

    Wazazi wanaopeleka watoto kwenye vituo vya malezi wana uhakika wa kupata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu za wiki, bila kupitia mchakato wowote wa uthibitishaji. Ruzuku hii itagharimu karibu dola milioni 430 kwa kipindi cha miaka minne ijayo, lakini serikali inasema mamia ya maelfu ya familia zitafaidika.

  • Taarifa ya habari:Maduro na mkewe wakanusha mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya na silaha jijini New York

    06/01/2026 Duración: 12min

    ** Rais wa Venezuela Nicolas Maduro na mkewe walikana hatia katika mahakama ya Marekani. ** Mtu anayedaiwa kuwa mfyatuliwa wa risasi Bondi amehamishwa kwenda gereza la Goulbourn supermax. **Na Denmark yaendelea kuikashaifu Marekani kuhusu manoni yao ya Greenland.

  • Yaliyojiri Afrika:Ushahidi mpya waonyesha kuwepo kwa jeshi la Rwanda DRC

    05/01/2026 Duración: 08min

    Jason anatujuza yanayojiri pande mbali mbali Afrika, Kwa habari zaidi elekea kwa tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Nini kipya mwaka 2026?

    05/01/2026 Duración: 08min

    Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Ukosefu wa maji wawaathiri wakaazi wa Tanzania

    05/01/2026 Duración: 08min

    Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Waasi wa M-23 kujiondoa ili kusaidia juhudi za amani Congo

    05/01/2026 Duración: 08min

    Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Burundi kuanza kusafirisha madini nje ya nchi ili kuimarisha uchumi

    05/01/2026 Duración: 08min

    Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Wanafunzi 300 waachiliwa baada ya kutekwa nyara shuleni Nigeria

    05/01/2026 Duración: 08min

    Kwa taarifa zaidi elekea katika mitandao yetu ya kijamii au pia tovuti yetu sbs.com.au/swahili.

  • Yaliyojiri Afrika:Hatua ya Israel kuitambua Somali Land yazua utata

    05/01/2026 Duración: 06min

    Mwanahabari Jason Nyakundi atujuza yaliyojiri Afrika. Kwa maelezo zaidi elekea kwa mitandao yetu ya kijamii au tovuti yetu sbs.com.au/swahili

  • Makala leo:YWCA yapewa sifa kwa kuwasaidia wanawake Sydney

    05/01/2026 Duración: 04min

    Kukusanya fedha ili kupunguza makazi duni miongoni mwa wanawake ndiyo lengo la hoteli moja mjini Sydney, moja kati ya biashara elfu kumi na mbili ya kijamii nchini Australia zinazochanganya faida na lengo. Likizo za kiangazi ni wakati wenye mafanikio kwa maeneo mengi ya utalii. Lakini hoteli ya Song mjini Sydney inazingatia zaidi ya kutengeneza pesa. Inasaidia miradi ya makazi ya YWCA kwa wanawake wanaohitaji msaada. Meneja Mkuu Jon Ackary anaeleza.

  • Makala leo:China yaongeza ushuru kwa bidhaa za nyama ya ng'ombe

    05/01/2026 Duración: 05min

    Biashara ya nyama ya ng'ombe ya dola bilioni ya Australia inakabiliwa na mabadiliko makubwa kutokana na hatua ya China kuweka ushuru wa asilimia Hamsini na tano kwa uingizaji wa bidhaa zinazozidi vikomo vya kila mwaka vilivyowekwa kwa ukali. Wakati serikali ya China inadai kuwa hatua hiyo inalenga kuwalinda wakulima wake dhidi ya usambazaji usiokuwa na kipimo, viongozi wa sekta ya Australia na Upinzani Mkuu wanatoa onyo kuwa nyongeza hii ya ushuru inakiuka makubaliano ya biashara huru baina ya Australia na Chini ya muda mrefu.

  • Taarifa ya habari:Marekani yavamia Venezuela na kumkamata rais Maduro na mkewe

    05/01/2026 Duración: 09min

    Rais wa Marekani Donald Trump ameamuru shambulio kubwa dhidi ya Venezuela kuwakamata Rais wa Venezuela Nicolás Maduro na mke wake. Wametuhumiwa na makosa ya dawa za kulevya na silaha huko New York. Hatua hiyo imepongezwa na washirika wa Bw. Trump, lakini imelaaniwa sana na mataifa mengi.

  • Tukio la risasi Sydney:wengi wauawa akiwemo mtoto mmoja, huku wengine wakijeruhiwa.

    15/12/2025 Duración: 10min

    Polisi wametangaza shambulio la risasi nyingi huko Bondi Beach Jumapili kama shambulio la kigaidi, baada ya wanaume wawili kufyatua risasi kwa mamia ya watu waliokusanyika kwa ajili ya sherehe ya Hanukkah. Watu wasiopungua 16 wameuawa, pamoja na mtoto, katika shambulio la risasi nyingi lililosababisha vifo vingi zaidi nchini Australia tangu mauaji ya Port Arthur ya mwaka 1996. Tukio hilo limezua shutuma za kimataifa, limeongeza usalama kwenye maeneo ya Kiyahudi, limeleta hofu miongoni mwa jamii na kuzusha tena wito kutoka kwa viongozi kukemea chuki na kusimama pamoja kwa mshikamano na jamii ya Kiyahudi.

  • Waaustralia wakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha

    11/12/2025 Duración: 07min

    Ripoti mpya ya kitaifa imegundua kuwa Waasutralia wanakabiliwa na wastani wa kusubiri miaka mitano kwa teknolojia za matibabu zinazookoa maisha. Ripoti inasema kuwa ingawa teknolojia za matibabu zinakua kwa kasi nje ya nchi, mfumo wa Australia bado uko polepole katika kupitisha na kufadhili teknolojia hizo mpya.

  • Matokeo ya Cronulla 2005 yakumbukwa kwa hisia mchanganyiko

    11/12/2025 Duración: 08min

    Miaka ishirini iliyopita, maelfu walikusanyika kwenye kitongoji cha pwani cha Cronulla huko Sydney, kwa kile kilichogeuka kuwa mkutano wa vurugu dhidi ya uhamiaji kutoka Mashariki ya Kati. Leo hii, wakazi wa Cronulla na baadhi ya Waaustralia wenye asili ya Mashariki ya Kati wanasema mitazamo inabadilika. Lakini wengine wanahofia kuhusu harakati mpya zaidi zilizo na mpangilio wa kupinga uhamiaji.

  • Wataalamu waonya kuwa msimu wa moto umeanza tunapotarajia joto kuongezeka

    11/12/2025 Duración: 08min

    Katika wiki za hivi karibuni, moto wa nyika umesababisha uharibifu wa nyumba na mali katika maeneo ya pwani ya katikati ya kaskazini ya New South Wales, Geraldton huko Magharibi mwa Australia na mashariki mwa Tasmania. Wataalamu wanaonya kuwa huu ni mwanzo tu wa msimu wa moto na nyinyi ambao mnasafiri kwa ajili ya likizo mnahitaji kuwa na ufahamu na maandalizi mkiwa mbali na nyumbani.

  • Baraza la usalama wa chakula latoa vidokezo jinsi ya kuandaa vyakula kwa usalama ili kuepukana na magonjwa

    11/12/2025 Duración: 06min

    Kuna mambo mengi ya kushughulikia wakati huu wa mwaka, na milo yetu inaweza kuja na upande wa magonjwa. Baraza la Habari za Usalama wa Chakula la Australia limetoa vidokezo vyake bora jinsi ya kufurahia msimu kwa usalama - kwa lengo la kupunguza zaidi ya kesi milioni nne na laki tano za sumu ya chakula kila mwaka.

página 1 de 34