Sbs Swahili - Sbs Swahili

  • Autor: Vários
  • Narrador: Vários
  • Editor: Podcast
  • Duración: 134:18:54
  • Mas informaciones

Informações:

Sinopsis

Listen to interviews, features and community stories from the SBS Radio Swahili program, including news from Australia and around the world. - Sikiza mahojiano, makala na hadithi za jumuiya kutoka Idhaa ya Kiswahili ya SBS Radio, ikijumuisha taarifa za habari kutoka Australia na ulimwenguni.

Episodios

  • Idadi ya watoto wa mataifa ya kwanza gerezani yazua tashwishi

    11/11/2025 Duración: 08min

    Serikali ya majimbo na maeneo nchini Australia zitachunguzwa kama sehemu ya uchunguzi wa bunge kuhusu matokeo na athari za kifungo kwa vijana. Kati ya maswala ya kuzingatia katika uchunguzi huu ni Kuzidishwa kwa kufungwa kwa watoto wa Mataifa ya Kwanza.

  • Serikali kudhibiti mitandao ya kijamii kuanzia desemba

    11/11/2025 Duración: 06min

    Mtandao wa Reddit na jukwaa la Kick zitaongezwa kwenye majukwaa yanayohitajika kuzuia watumiaji walio na umri chini ya miaka 16, sheria mpya zitakapoanza kutekelezwa mwezi Desemba. Marufuku ya Australia ya mitandao ya kijamii kwa watoto chini ya miaka 16, ambayo inajumuisha majukwaa nane kuu, inategemea tathmini zinazoendelea za eSafety ambazo zinaweza kufafanua kati ya huduma za mitandao ya kijamii, ujumbe, na michezo, kuelezea ni kwanini majukwaa kama Steam na Twitch hayakujumuishwa. Wakati serikali ilihakikishiwa na Roblox kwamba wataanzisha teknolojia za kuthibitisha umri ili kupunguza tabia za uwindaji wa watoto, watetezi wa haki za kidigitali wanatahadharisha kwamba marufuku haya yanaweza kuhamasisha watoto kutumia majukwaa madogo yasiyo na uangalizi ambapo wanaweza kukumbana na madhara makubwa zaidi.

  • Viza ya milioni moja kutolewa nchini Australia

    11/11/2025 Duración: 07min

    Australia inatarajia kutoa kibali cha kila kudumu ama permanent humanitarian visa , cha milioni moja tangu kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwisho wa mwaka huu. Hatua hii imewezesha sherehe juu ya mchango mkubwa ambao wakimbizi hufanya katika hadithi ya kitaifa ya Australia. Lakini mashirika ya haki za wakimbizi yanasema ni wakati muafaka kufikiria jinsi Australia inaweza kuboresha jibu lake kwa ukimbizi mkubwa wa dunia nzima.

  • Mfumo wa utoaji wa mayai ya uzazi Australia huenda ukabadilika

    11/11/2025 Duración: 08min

    Mahitaji ya mayai ya uzazi yanaongezeka nchini Australia kadiri watu wanavyokumbwa na changamoto za uzazi. Lakini mahitaji ya mayai ni makubwa mno kuliko upatikanaji wao na sasa, wataalamu wanapendekeza Australia ifikirie kubadilisha kanuni zinazohusu utoaji mayai.

  • Afya ya akili:kupata usaidizi kama mhamiaji

    10/11/2025 Duración: 08min

    Wahamiaji wengi wanakumbana na matatizo tofauti wanapojaribu kupata msaada wa afya ya akili. Umoja wa Mataifa unasema kwamba upatikanaji wa huduma za afya ya akili ni haki ya msingi kwa kila mtu , ikiwemo wahamiaji na wakimbizi. Umoja wa Mataifa unasisitiza kwamba wahamiaji mara nyingi wanakabiliwa na changamoto nyingi kama vile msongo wa mawazo, huzuni, kiwewe na ata upweke kutokana na mazingira mapya. Mtaalamu wa Afya ya Akili Terry Kiguru anatueleza jinsi ya kupata msaada huo na kwanini.

  • Jamii ya Sudan walio Australia waendelea kuwa na wasiwasi

    10/11/2025 Duración: 08min

    Jamii ya watu wa Sudan walio nchini Australia wana wasiwasi mkubwa ,wakisubiri habari kutoka kwa familia zao walionaswa katika jiji la Al-Fasher baada ya mlipuko wa ghasia. Jiji hilo lilitekwa na Rapid Support Forces wiki mbili iliyopita, na wataalamu wanaamini kwamba maelfu huenda wameuawa katika mauaji ya kutisha. Kwa kuwa huduma za intaneti na simu zimekatwa, wanaoishi nje ya nchi wanalazimika kukaa na kusubiri ili kujua kama wapendwa wao bado wako hai.

  • Umaskini wa nishati

    10/11/2025 Duración: 07min

    Maelfu ya kaya za Wenyeji kaskazini mwa Australia wanaishi na mfumo wa kulipa kabla wa umeme, ambapo kukatwa kunaweza kutokea wakati wowote. Ripoti mpya sasa imeonya kwamba bila ulinzi wa kutosha, mfumo huu unaweza kuwa hatari katika joto kali.

  • Hali ya hewa inawaathiri pinguini

    08/11/2025 Duración: 05min

    Timu ya kimataifa ya wanasayansi imeonya kuwa pIngwini wanaweza kuwa katika hatari kutokana na madhara ya hali mbaya ya hewa. Utafiti mpya unapendekeza kwamba si tukio moja kama vile joto kali inayosababisha hatari kubwa zaidi, bali ni athari zake zilizoungana pamoja katika ardhi na baharini.

  • Mzio wa karanga kwa watoto upata mwelekeo mpya

    04/11/2025 Duración: 07min

    Miaka kumi baada ya utafiti muhimu kudhibitisha kwamba kuwalisha watoto wachanga bidhaa za karanga inaweza kuendeleza mzio hatari, utafiti mpya umebaini kuwa kuna uwezekano wa kuepuka kuendeleza mizio ya chakula.

  • Serikali kudhibitisha umuhimu wa wahamiaji kwenye uchumi

    04/11/2025 Duración: 05min

    Waziri wa Mambo ya Ndani, Tony Burke, anasema kwamba serikali inafanya kazi juu ya uwezekano wa kutambua ujuzi wa nje ya nchi. Anasema hii itasaidia kuokoa muda na pesa kwa wahamiaji wenye ujuzi wanaotafuta kuhamia Australia. Katika hotuba yake kwa Klabu ya Waandishi wa Habari huko Canberra, Bw. Burke pia ametangaza mabadiliko kwenye akaunti za benki zisizotumika ili kukabiliana na utakatishaji wa fedha.

  • Understanding treaty in Australia: What First Nations people want you to know - Mkataba wa amani: Una maana gani na Una manufaa gani

    04/11/2025 Duración: 05min

    Australia is home to the world’s oldest living cultures, yet remains one of the few countries without a national treaty recognising its First Peoples. This means there has never been a broad agreement about sharing the land, resources, or decision-making power - a gap many see as unfinished business. Find out what treaty really means — how it differs from land rights and native title, and why it matters. - Waingereza walipowasili Australia walitangaza ardhi kuwa ‘terra nullius’ kumaanisha ardhi isiyomilikiwa na yeyote. Hawakuona haja ya kuzungumza na mataifa ya waaboriginals na kwa hivyo wenyeji wa Australia wanasema kwamba hii ni biashara ambayo haijakamilika.

  • Taarifa ya Habari 26 Septemba 2025

    26/09/2025 Duración: 14min

    Waziri wa Mambo ya Nje Penny Wong amesema Australia ina simama kidete juu ya tamaduni nyingi, baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kukosoa uhamiaji katika hotuba yake kwa kikao cha mkutano wa Umoja wa Mataifa.

  • Taarifa ya Habari 23 Septemba 2025

    23/09/2025 Duración: 17min

    Waziri Mkuu amesema ombi la utaifa wa Palestina ni fursa ya amani, katika hotuba yake kuhusu soluhu ya nchi mbili, alipo hudhuria kikao cha Umoja wa Mataifa hii leo Jumanne 23 Septemba 2025.

  • Serikali ya shirikisho yazungumza kwa ukali baada ya kupotea kwa huduma ya simu ya dharura ya Optus

    23/09/2025 Duración: 09min

    Waziri wa Shirikisho wa Mawasiliano amesema Optus inastahili tarajia adhabu kubwa, kufuatia kupotea kwa huduma ya namba ya dharura ya 000, hali ambayo ime husishwa na vifo kadhaa.

  • Kamerhe chini ya shinikizo kuondolewa kama spika wa bunge la DRC

    22/09/2025 Duración: 06min

    Taratibu zinazolenga kumfuta kazi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Vital Kamerhe zinaendelea huku kukishuhudiwa hali ya mfarakano kati ya rais Félix Tshisekedi na mshirika wake huyo wa zamani.

  • Taarifa ya Habari 19 Septemba 2025

    19/09/2025 Duración: 14min

    Kampuni ya pili kwa ukubwa ya madini imetangaza inapunguza ajira. Anglo American Australia imesema ita angaza kupunguza idadi ya wafanyakazi Queensland, na takriban wafanyakazi 200 wata athirika.

  • Raia wapya wa Australia wakaribishwa katika sherehe katika Siku ya Uraia ya Australia

    19/09/2025 Duración: 11min

    Maelfu ya watu wanasherehekea kuwa raia wapya wa Australia, katika sherehe zilizo andaliwa na halamshauri za jiji kote nchini kwa siku ya Uraia wa Australia.

  • SBS Learn Eng Ep 93 Namna ya kujigamba kuhusu gari lako katika Kiingereza

    19/09/2025 Duración: 16min

    Je, unajua jinsi ya kujigamba kuhusu gari lako?

  • Taarifa ya Habari 16 Septemba 2025

    16/09/2025 Duración: 15min

    Naibu Waziri Mkuu Richard Marles amekana madai kuwa uwekezaji wa $12 bilioni iliyo tangazwa juzi ime undwa ili kutuliza maombi ya Marekani kwa Australia kuongeza matumizi yake katika ulinzi.

  • SBS Learn Eng Ep 95 Anga la usiku

    16/09/2025 Duración: 13min

    Je, unajua jinsi ya kuelezea kuhusu anga la usiku?

página 4 de 34